Mtu mwenye good Communication Skills, Makini na Charisma anaweza kuwa MSEMAJI. Ila inapokuja kwenye usemaji unaohusisha maswala technical, Msemaji wake anapaswa awe na weledi, ujuzi, uzoefu na exposure ya swala hilo
Steve Nyerere is charismatic & Influential. Ni mtu mzuri (hanaga baya) ila anakosa vigezo ambavyo ni muhimu zaidi kuliko hiyo Charisma na Ushawishi wake.
Isitoshe viongozi hawajampa tu Usemaji bali pia ni “Chief Strategist” of Music Federation. To put it in context, mtu wa Mipango, Mikakati, Allocation ya Funds, Vision, etc Dah!
Mtu ambae kila kitu anachukulia Mzaha, kweli ndio abebe vision na hatma ya Wasanii nchini?
Tuna mambo very crucial na yapo kwenye critical point. Huu ni muda wa kuwa na viongozi na wasemaji ambao watatuvusha with utmost seriousness and we are hiring a COMEDIAN with political ambitions. Can he even communicate the needs of Artists & Producers?
Sasa badala ya kum-crucify “Tivu ake”, I think we should point fingers kwa viongozi wa Shirikisho waliomchagua. Rais (Addo November), Makamu (Mzee Yusufu) na Katibu Mkuu (Fid Q). Wengine hao siwajui vizuri, ila sisi tulimuamini sana Fareed kutokana na umakini wake. WHY, HOW?
It is either Viongozi ni incompetent na hawajui watendalo, au wamefanya hivyo kwa makusudi with a hidden agenda and motive behind. Is it politically driven? Wanataka awasaidie kupata hela sehemu? Sijui ila nachojua ni kwamba wameidhalilisha Tasnia, Shirikisho na wao wenyewe!! I think Viongozi wa Shirikisho wawajibike wao kwanza, then Basata/Wizara iitishe mkutano wa Dharura wa kuchagua uongozi mpya.
TUMA wanapaswa kutoa Tamko la kupinga na kuhamasisha Wasanii wake kuji-mobilize ili kuweka pressure BASATA!
Kwanza huu uteuzi ni batili, maana Nafasi hiyo kwa mujibu wa Katiba ya Shirikisho ni ya Kuchaguliwa kwa Kura na Siza Mazongera ndio alishinda. Sasa inaonyesha viongozi wanaibagaza Katiba na kufanya watakavyo au wanaibadilisha pasi na sisi kufahamu mchakato.
Mimi SITAKI HIYO NAFASI. Ila nawajua Wasanii wanaoweza kuifanya kwa ufanisi zaidi ya Tivu: Fid Q, Baghdad, Witness, Brayton, Fanani, Soggy Doggy, Freshlikeuhhh, Baby Madaha, Bushoke, P Funk, Davie Machord, One Incredible, MwanaFA, etc