Wakazi "Nina Muelewa sana Nay Kujitoa Katika Tuzo ingawa Sidhani Kama ni Maamuzi Sahihi"



Ameandika Wakazi:

Kwenye group la Wasanii nilitoa wazo la sisi ku-Boycott Tuzo ikiwa Steve Mengele na Uongozi wa Shirikisho hautaachia ngazi. Ila sikupata Support kubwa. ila Siku iliyofuata, Nay Wa Mitego alijitoa kwenye Tuzo kwa sababu za kuona mapungufu kwenye Tuzo hizo za TMA. Nina muelewa sana, ingawa sidhani kama ni maamuzi sahihi kama nia ni kuboresha TUZO.

Miaka 8 hamna Tuzo nchini, alafu tukawa tunajidanganya “Muziki wetu umekua”. Nchi ambazo Muziki ni mkubwa au umekua, kuna Tuzo 20 kidogo. There was a dire need to brick back these Awards. (Wizara, Waziri Bashungwa, Waziri Mchengerwa, Katibu Mkuu Dkt Abbasi, Cosota, Basata na Watendaji wake wanastahili pongeza kwa hatua hii) But let’s get realistic kidogo:

Kurudi kwa Tuzo ni kitu cha msingi sana? bila shaka. Tuzo zina mapungufu? haipingiki. Waandaaji wamejitahidi kupokea mawazo ya uboreshaji? without a doubt. Kuna baadhi ya Mapungufu ni ya kizembe? absolutely. Kuna baadhi ya Mapungufu yanaweza rekebishika kwa sasa? Bila shaka. Kuna makosa mengine ya kiufundi yanahitaji kusubiria mwakani? Kabisa. Wasanii tunahitaji kuzisupport Tuzo? yes indeed.

Vitu visipokaa sawa, alafu wewe unaona kabisa vingeweza kukaa kama wangekuwa makini kidogo, huwa ina frustrate. Ndio maana ninamuelewa Nay Wa Mitego kwa maamuzi aliyochukua. ILA upande wa pili, uwepo wa Tuzo ni muhimu zaidi, so badala ya kuzisusia na kufanya pengine ziondoke tena, ni bora kushiriki na kuendelea kudai maboresho as we go. Hii sio tu kwa Nay, ila na baadhi ya wasanii wengine ambao walisusia kushiriki. Tuweke Muziki/Sanaa mbele na sio maslahi yetu binafsi. Mimi nauweka Muziki mbele, bila mimi Album ya Marco Chali isingekuwepo kwenye Nominees, ila nilipambana aiweke (maana hakuwa na taarifa) huku nikijua fika anaenda kuwa mpinzani wangu kwenye Category! Lets put the music first, and then katika maboresho ya Tuzo tutumie HOLISTIC APPROACH going forward…

Nimeona niseme hili, isije kuonekana nakalia kimya kisa ni Nominee… I never put myself above the cause, ila pia on this, kususia sio the right course of action. Kwa mapungufu yanayoweza kurekebishika nitafikisha ujumbe @basata.tanzania kupitia available channels.

The Leader.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad