Wakili Ajitoa Kumtetea Mshitakiwa Kesi ya Sabaya



Arusha. Wakili wa mmoja wa watu wanoshtakiwa pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya kwa uhujumu uchumi na utakatishaji fedha amejiondoa kumtetea mteja wake.

Wakili Fridoline Bwemelo amesema ameamua kujiondoa kumtetea mshtakiwa wa tatu katika kesi hiyuo, Watson Mwahomange kwa kile alichodai kuwepo mgongano wa kimaslahi na kulinda maadili yake.

Bwemelo ameeleza uamuzi huo leo Jumatatu Machi 7, 2022 mbele ya Hakimu mkazi Mwandamizi, Dk Patricia Kisinda.

Alidai kuna mambo ambayo mshitakiwa huyo alimtaka ayaeleze mahakamani lakini akaona asingeweza kufanya hivyo kutokana na maadili yake ya kitaaluma.


”Mimi kwa kiapo changu kama ofisa wa mahakama sikuwa tayari kukieleza hicho ambacho naona kitaende kinyume na maadili yangu kama wakili au ofisa wa mahakama,” amesema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad