Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Jijini Dar es salaam, imetoa siku 21 kwa aliyekuwa RC wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kuwasilisha hati kinzani dhidi ya maombi yaliyofunguliwa na Mwanasiasa Saed Kubenea.
Hatua hiyo imefikiwa mbele ya Hakimu Mkazi, Aron Lyamuya, baada ya Makonda kutuma Mwakilishi ambaye ni Wakili wake, Goodchance Reginald Hakimu Lyamuya ametoa amri hiyo baada ya Wakili Reginald kuomba muda wa kujibu maombi akidai mteja wake hakupata wito wa mahakama "Mteja wangu (Makonda) aliniambia hakupata taarifa yeyote ya wito, imgependeza tungepata wito ili tuwe na muda wa kujibu"
Hata hivyo, ombi hilo lilipingwa na Wakili wa Kubenea, Hekima Mwasipu, akidai kuwa hajaiambia Mahakama Makonda taarifa imemfikiaje hadi yeye amekuja Mahakamani kumwakilisha ambapo katika majibu yake, Wakili Reginald amesema "Mteja wangu alipata hizi habari kupitia vyombo vya habari, akaona sio vizuri yeye alikuwa Kiongozi wa Serikali akaona ni alete uwakilishi lakini wito hajapewa."
Kesi hiyo imeahirisha hadi March 25, 2022 ambapo wajibu maombi wataleta hoja za mapingamizi yao.