Wanaume nchini Ukraine wamebainika kujificha kwenye buti za magari katika majaribio ya kutoroka ili kuyanusuru maisha yao licha ya Serikali kuwapiga marufuku Wanaume wenye umri wa miaka 18 na zaidi kuondoka nchini humo ili wasaidie mapambano ya kupigania Nchi yao dhidi ya vikosi vya Urusi.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ukraine imesema baadhi ya Wanaume wanajifanya ni Raia wa kigeni huku wengine wakijaribu kuwahonga Walinzi wa mipaka ili wakimbie Nchi.
Mwanaume mmoja aligunduliwa kwenye buti la gari la Mkewe aina la Lexus kwenye kizuizi cha mpakani huko Luzhanka, kwenye mpaka wa Hungary na Ukraine na mwingine alikutwa akiwa amejificha kwenye buti ya gari aina ya Mitsubishi baada ya kujaribu kuwalipa Walinzi wa mpaka.
Mtu mwingine alidandia treni na kujaribu kuvuka mpaka bila kupata kibali cha Maafisa wa mpakani.