Watanzania 2 wahukumiwa miaka 35 Jela Nchini Kenya




Mahakama kuu ya Migori nchini Kenya imewahukumu raia wawili wa Tanzania kifungo cha miaka 35 kila mmoja kwa kosa la mauaji ya mwajiri wao.

Watanzania hao ni Marwa Magige Kieusi na Makonge Wangwi Maseti ambao wote walipatikana na hatia ya mauaji ya Thomas Moronge Makuri mnamo Juni 2020 kwa sababu zisizojulikana.

Makuri alikumbana na kifo chake cha ghafla kati ya Juni 5, 2020, na Juni 6, 2020, katika kijiji cha Karosi huko Bukira Mashariki, eneo dogo la Kuria Magharibi ndani ya kaunti ya Migori.

Taarifa za polisi zinasema wafungwa hao walitumia silaha butu ikiwemo panga na kisha kutupa mwili ndani ya tanki la maji la chini ya ardhi ndani ya boma hilo na baadaye walitorokea nchini Tanzania.


 
Baada ya msako wa Polisi wa upelelezi wa Kenya, Kieusi na mshtakiwa mwenzake Makonge walikamatwa nchini Tanzania kwa nyakati tofauti na kusindikizwa hadi Kenya kujibu shtaka la mauaji mbele ya Mahakama Kuu ya Migori ambapo walikana mashitaka hayo.

Kesi hiyo ilianza rasmi Novemba 23, 2020, mbele ya Hakimu Roseline Wendo na Upande wa mashtaka ulifunga kesi hiyo Aprili 24, 2021 baadae kesi hiyo ilipangwa kutajwa Mei 20, 2021, na washukiwa wakatakiwa kujitetea kutokana na makosa yaliyokuwa yakiwakabili.

Washtakiwa hao wawili walipatikana na hatia ya mauaji na Mnamo Februari 24, 2022, kila mmoja alihukumiwa kifungo cha miaka 35 jela.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad