Wataokafaulu masomo ya sayansi kidato cha sita kusomeshwa nje ya nchi




Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolph Mkenda
Dar es Salaam. Ili kuchochea ufaulu katika masomo ya sayansi Serikali imesema itatoa udhamini kwa wanafunzi watakofanya vizuri katika masomo hayo katika mitihani ya kidato cha sita kwenda kusoma nje ya nchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolph Mkenda wakati akielezea mafanikio na utekelezaji wa wizara hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan madarakani.

Amesema kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020 ya kudhamini wanafunzi wanaofanya vizuri katika masomo ya Biolojia, Kemia na Fizikia watapelekwa kusoma nje ya nchi katika vyuo bora zaidi duniani chini ya Serikali.

"Tutahakikisha wanafunzi wanaofanya vizuri kidato cha sita kwenye masomo ya Sayansi, tutachukua baadhi yao wanaofanya vizuri zaidi na kuwapeleka moja kwa moja kwenye vyuo bora zaidi duniani kwenda kusoma na watasomeshwa na Serikali," amesema.


 
Waziri huyo amesema katika kufanikisha hilo wanazungumza na Watanzania wanaokaa nje ya nchi Ili kuongeza udhamini huo.

Amesema Serikali imeongeza bajeti ya elimu kwa watu wenye mahitaji maalumu ili kutoa fursa ya wote kusoma.

“Kwenye bajeti ya Wizara tumeongezewa fedha na na zimewezesha kuchapisha vitabu vingi zaidi kwa wanafunzi wenye uoni hafifu, tumenunua vishikwambi na viti mwendo kwa watoto changamoto ya ulemavu,” amesema huku akizitaja shule zilizojengwa kwa wenye mahitaji maalumu kuwa ni Lukalen ya Mtwara, Patandi ya Arusha na nyingine iliyopo Geita.


Amesema Serikali imejenga vituo shikizi 3, 000 nchi nzima Ili kutoa nafasi ya watoto waliopo katika maeneo ya mbali na shule kupata huduma ya elimu na vinasimamiwa na shule zilizopo katika maeneo hayo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad