Wizara ya Afya imesema kuanzia Februari 5, 2022 hadi Machi 4, 2022 kumekuwa na visa vipya 290 vya COVID-19, huku Dar es Salaam ikiongoza kwa kuwa na Wagonjwa 175.
Katika kipindi hicho Wagonjwa 136 walilazwa ambapo 128 kati yao hawakuwa wamepata chanjo dhidi ya Virusi vya Corona, huku Vifo vikiwa nane.
Serikali imesema hadi sasa watu 2,664,373 wamepata Dozi kamili ya kujikinga na Virusi vya Corona.