Waziri Mkuu mstaafu Mali afariki kizuizini



WAZIRI MKUU mstaafu wa Mali, Soumeylou Boubèye Maïga amefariki dunia jana tarehe 21 Machi, 2022 katika hospitali moja iliyopo jijini Bamako.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Serikali ya kijeshi iliyochukua madarakani nchini humo, ilitoa salamu za pole kwa familia ya kiongozi huyo. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Hata hivyo, mmoja wa ndugu wa karibu wa familia hiyo amelieleza Shirika la Habari la Reuters kuwa hali yake kiafya ilianza kuzorota kutokana na mazingira ya kuzuiliwa kwake.

Kiongozi huyo alilazwa hospitalini takriban miezi mitatu iliyopita, lakini daktari wake kushauri apelekwe nje ya nchi kwa matibabu, serikali iliyopo madarakani haikuruhusu.

Waziri Mkuu huyo alikamatwa na kisha kuwekwa chini ya waranti ya kukamatwa Agosti mwaka jana, kama sehemu ya uchunguzi wa tuhuma za rushwa katika ununuzi wa ndege ya Rais wa nchi hiyo, Ibrahim Keita ambaye litimuliwa madarakani na jeshi mapema mwaka huu.

Aidha, Maiga ambaye awali alikuwa waziri, aliteuliwa kushika nafasi ya waziri mkuu mwaka 2017 kisha akajiuzulu baada ya miaka miwili kutokana mauaji ya watu 160 kutoka kabila linalofahamika kwa jina la Fulani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad