Waziri wa Afya Ummy Mwalimu Atoa Tahadhari ya Kuzuka kwa Ugonjwa wa Homa ya Manjano (Yellow Fever)


Waziri wa Afya Tanzania Ummy Mwalimu ametoa tahadhari ya kuzuka kwa ugonjwa wa Homa ya Manjano (Yellow Fever) na kusema tarehe 3 March 2022 Wizara ilipokea taarifa kutoka WHO hapa nchini ikielezea kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa homa ya manjano nchini Kenya.

Waziri Ummy amesema hadi tarehe 03 Machi 2022 nchini Kenya kulikua na wagonjwa wa Homa ya manjano 15 na vifo vitatu (3) ambapo katika sampuli sita zilizopimwa maabara ya Kenya kwa kutumia vipimo vya serology na PCR sampuli 3 zilithibitika kuwa na maambukizi.

"Hapa nchini taarifa ya kipindi cha miezi mitatu iliyopita katika mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa zinaonesha kuwa hakuna taarifa zinazoashiria kuwepo kwa ugonjwa wa homa ya manjano, pia taarifa za ufuatiliaji wa tetesi za magonjwa haujaashiria kuwepo kwa ugonjwa huo" ——— Waziri @UmmyMwalimu
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad