Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba Aanika Bajeti ya 2022/23



Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba leo Ijumaa, Machi 11, 2022 jijini Dodoma amesema, Serikali inapanga kutumia Tsh trilioni 41 kwa mwaka wa fedha 2022/23 ikiwa ni ongezeko la takribani Tsh Trilioni 5.

Mwigulu amesema hayo wakati akiwasilisha mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Ukomo wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 ambapo serikali inakusudia kukusanya na kutumia Sh trilioni 41.06.

Ikumbukwe kuwa, Bajeti ya mwaka wa fedha 2021/22 ilikuwa Tsh 36.3.

Katika Taarifa ya Nchemba, kiasi cha Tsh trilioni 28 sawa na asilimia 70 ya mapato kitatokana na makusanyo ya ndani.


Kwa mujibu wa Waziri wa Fedha, Bajeti ya mwaka ujao itagusa maendeleo ya Jamii hususani sekta ya Kilimo ambayo itatengewa kiasi kikubwa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad