Wezi Waiba na Kubaka Kanisani


Polisi nchini Afrika Kusini wameanza msako mkali katika mji wa Mpumalanga dhidi ya washukiwa watatu waliovamia kanisa moja lililopo Thulamahashe karibu na Bushbuckridge na kuwabaka wanawake wawili kisha kuondoka na gari la mchungaji pamoja na vyombo vya muziki.

Kwa mjibu wa polisi tukio hilo limetokea Machi 18 mwaka huu majira ya saa tano usiku wakati wanawake hao waliokuwa kwenye chumba kimoja ndani ya kanisa hilo, wakisikia mlio wa risasi kisha mlango ukagongwa ambapo walishangaa kuona watu watatu wakiwa na silaha wakiingia ndani kwa nguvu.

Pamoja na hilo washukiwa hao pia walichukua vyombo vya muziki vya kanisa hilo vyenye thamani ya takribani Sh milioni 4.3 (R28,000), wakitumia gari aina ya KIA Picato ya rangi ya silver, mali ya Mchungaji wa kanisa hilo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad