Will Smith(53) ashinda tuzo yake ya kwanza ya Oscars/Academy award ya mwigizaji bora wa mwaka, amzabua Chris Rock kwa kumtania mkewe
Kupitia filamu ya King Richard ambayo ameigiza kama baba yake kina Venas na Serena Williams akiwanoa mabinti zake kuhusu mchezo wa Tennis, ameshindwa tuzo ya mwigizaji na kuwabwaga wapinzani wake akiwemo Denzel Washington, hata hivyo Will Smith tangu mapema alipewa nafasi kubwa zaidi ya kushindwa tuzo hiyo kwani perfomance yake ilikubalika sana na kutawala tuzo nyingine kabla. Akitoa speech alipatwa na hisia hadi kumwaga chozi
Kwa upande mwingine, kabla ya kutangazwa kuwa kushinda tuzo hiyo, Will amlizaba kibao Chris Rock(57) aliyekuwa mtangazaji wa tuzo hizo baada ya kumtania Jada Pinkett Smith(50) kuhusu mtindo wake wa nywele wa upara
Chris Rock alisema, alisema anampenda Jada huku akisema anaisubiri sehemu ya 2 ya filamu ya G.I.Jane utani huo akiulekeza kwa Jada kuhusu style ya nywele ya upara. Kwa ambao hawajaelewa. G.I. Jane ni filamu ya mwaka 1997 iliyomuonesha mwigizaji Demi Moore akiwa na upara
Mwanzo wa utani huo Will Smith alichukulia poa na kutabasamu, lakini Chris Rock alipoendelea Will Smth hakupendezwa na hata Jada alionekana kupandwa na hasira kwasababu miaka ya karibuni Jada amekuwa akipambana na tatizo la kupoteza nywele(Alopecia) hadi baadaye akaamua kuanza kujikubali na kuonyoa upara na kuwa advocate wa tatizo hilo hadharani hivyo utani huo hakupendezwa
Will Smith alipanda jukwaani kumzaba kibao Chris Rock kisha kumwambia aache kumtajataja mkewe
Mwanzo baadhi ya watu walijua ni utani Ila baadaye wakaelewa Smith alikuwa serious hataki utani na mkewe
Baadaye nyuma ya jukwaa mastaa wenzie wakubwa akiwemo Denzel Washington na Tyler Perry walimfuata Smith kuongea nae
Baadaye aliyoshinda tuzo alichukua pia nafasi hiyo kuomba radhi kwa kumpiga Chris Rock live
Smith na Chris Rock tangu 2016 hawana maelewano mazuri sana kwani mwaka huo Chris Rock alikuwa pia mtangazaji na alimtania Jada Smith aliyekuwa mstari wa mbele kupaza sauti kugomea tuzo hizo kwa mwaka huo kushuka chini kwamba zilikuwa na ubaguzi sana kupendelea wazungu na kusahau vipaji vya watu weusi, madai ambayo kwasasa yanmeonekana kufanyiwa kazi