Yanga, Somalia zatoshana nguvu Chamanzi



Mchezo kati ya Yanga na timu ya taifa Somalia umemalizika kwa sare 1–1 katika uwanja wa Azam Complex huku asilimia 40 za mapato yatakayopatika yakienda kwenye mfuko wa Kimari.

MCHEZO wa hisani kwa ajili ya matibabu ya Ali Kimari kati ya Yanga dhidi ya timu ya taifa Somalia umemalizika kwa sare 1–1.

Mchezo huo umepigwa katika uwanja wa Azam Complex huku asilimia 40 za mapato yatakayopatika yakienda kwenye mfuko wa Kimari.

Dakika 45 kipindi cha kwanza timu hizo walizitumia vizuri baada ya kila mmoja kupata bao kwenye mchezo huo.

Somalia walikuwa wa kwanza kupata bao dakika 17 lakini bao hilo lilidumu kwa dakika sita tu.


 
Dakika 24 Chico Ushindi alifunga Yanga bao baada ya kuunganisha kwa kichwa krosi ya Djuma Shabani ambaye aliuchonga mpira kwa utulivu.

Dakika 28 Yanga ilikosa bao la pili baada ya Feisal Salum kuwatoka mabeki wa Somalia na kupiga shuti lakini mpira ulitoka nje kidogo ya lango.

Mchezo ulikuwa na utulivu kwa timu zote huku kila mmoja akionyesha kuhitaji bao la pili katika mchezo huo.

Dakika 54 Yanga ililazimika kufanya mabadiliko ya kumuingiza Dikson  Ambund baada ya Chico Ushindi kupata maumivu yaliyomfanya ashindwe kuendelea na mchezo.

Dakika 62 Yanga walifanya mabadiliko mengine ya kumtoa Heritier Makambo na kuingia Fiston Mayele ili kwenda kuongeza nguvu kwenye eneo la ushambuiaji.

Timu ya taifa Somalia walikuwa na utulivu kwenye mchezo huo na kucheza kwa nafasi wakiwa hawakai na mpira mguuni.

Dakika 75 Yanga nusra wapate bao la pili baada ya Ambundo kutuliza mpira ndani boksi na kupiga pasi kwa Denis Nkane ambaye shuti lake halikulenga lango.


 
Dakika 80 Yanga walifanya mabadiliko mengine ya kuwatoa Salum Abubakari na Djuma Shaban na nafasi zao wakiingia Zawadi Mauya na Kibwana Shomari.

Dakika 90 Fiston Mayele alipata nafasi ya kufunga bao la pili baada ya kuingia ndani ya boksi na kufyatuka shuti kali lakini kipa wa Somalia aliucheza na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad