Yanga Yaingia Vitani na Vigogo wa Morocco Kumpata Nyota wa Orlando



Klabu ya Yanga inahusishwa kwa kiasi kukubwa kuwania saini ya mchezaji wa Orlando Pirates Mhango Gabadinho. Mchezaji huyo raia wa Malawi pia anawindwa kwa kiasi kikubwa na klabu ya RS Berkane ya nchini Morocco.

Gabadinho ni moja ya mchezaji aliyefanya vizuri akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya Malawi katika michuano ya Afcon nchini Cameroon. Yanga wamekuwa wakimuwinda mchezaji huyu kwa kipindi cha muda mrefu sasa.

Inaonekana wameamua kuongeza nguvu ili kuhakikisha msimu ujao anakuja kucheza katika klabu ya Yanga. Klabu ya Orlando Pirates kwa sasa imekuwa haifanyi vizuri katika ligi ya nchini Afrika Kusini lakini pia katika mashindano ya kimataifa.

Hii inaweza kumfanya aamue kutafuta changamoto mpya katika timu nyingine. Yanga kwa sasa ni timu ambayo imejiimarisha vizuri kuanzia ndani ya uwanja mpaka nje ya uwanja.

Yanga watakuwa na vita kubwa ya kushindana na klabu ya RS Berkane ambayo inaonekana kuwa na uhakika mkubwa wa kumpata mchezaji huyu kutokana na nguvu kubwa ya kipesa waliyonayo.

Mkurugenzi mtendaji wa klabu ya Yanga Senzo Mazingiza aliwahi kunukuliwa akisema kuwa kwa sasa klabu ya Yanga inaweza kumsajili mchezaji yoyote ambaye mwalimu atamuhitaji ndani ya kikosi. Kwahiyo kumpata Gabadinho inaweza ikawa ni jambo rahisi kwa Yanga.

Yanga inataka kuboresha kikosi chake kwa kuwa tayari inanafasi kubwa ya kwenda kucheza michuano ya kimataifa kwa msimu ujao licha ya kuwa bado kuna ushindani mkubwa.


Kama Yanga watafanikiwa kumpata mchezaji huyu anaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika ligi lakini pia katika michuano ya kimataifa. Hamasa ya mpira wa Tanzania kwa sasa imekuwa kubwa ndiyo maana wachezaji wengi wamekuwa wakishawishika kuja kucheza mpira nchini Tanzania.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad