ZA NDAANI KABISA: Morrison anampisha Moses Phiri




 
ZA NDAANI kabisa ambazo hazina chembe ya shaka ni safari inamkuta Bernard Morrison ndani ya Simba hata afanyeje.

Ni kwamba Mzambia, Moses Phiri wa Zanaco ameshasaini mkataba wa awali na Simba ambao unaanza Agosti Mosi mwaka huu na wameshakubaliana kila kitu.

Simba walimsimamisha Morrison hivi karibuni lakini sasa wamemrejesha kikosini kwa sharti la kutakiwa kuonyesha kiwango cha juu ndani ya mechi mbili mfululizo na asikutwe na kosa lolote la utovu wa nidhamu. Usajili wa Phiri unamaanisha pia Yanga wamepigwa changa la macho kwani msimamizi wa staa huyo alikuwa na mawasiliano ya karibu nao akawaahidi watulie kwanza msimu umalizike Zambia.

Simba wamemrejesha Morrison ili awabusti kwenye mechi mbili ngumu za ugenini dhidi ya USGN na Berkane lakini jezi yake ataikabidhi kwa Phiri punde. Pia viongozi wamekubaliana watamchomoa mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu kwani wamejiridhisha si mtu sahihi kwao na amekuwa na makosa yanayojirudia ambayo hayavumiliki.


 
Mmoja wa vigogo wa Simba ameliambia Mwanaspoti Morrison ana uwezo mkubwa na amecheza kwenye kiwango chake akiibeba timu lakini amekuwa si mtu wa kutegemea kikosini kutokana na mienendo yake ambayo haiendani na gharama klabu ilizotumia dhidi yake kuanzia usajili mpaka mishahara.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad