ZA NDAANI KABISA: Wawa ndo basi tena



NI suala la muda tu. Mwisho wa msimu huu Simba itasajili wachezaji wanne wa kigeni ili kuongeza makali ya kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao.

Ili Simba ishushe majembe hayo akiwamo Victorien Adebayor wa USGN ya Niger ni lazima iwaache wengine ipatikane nafsi ya wapya kuingia, huku moja ya jina linalotajwa litakalokuwa la kwanza ni Pascal Wawa.

Kanuni ya usajili inaruhusu klabu kusajili wachezaji 12 wa kigeni na kwa sasa Simba imeshajaza, lakini mabosi wao wameanza kumalizana na nyota wapya ili watue Msimbazi na Wawa anahesabiwa siku.

Wawa ilikuwa aachwe mwishoni mwa msimu uliopita, ila kocha wa Simba, Didier Gomes aliwapa masharti magumu mabosi zake na suala la kumuacha beki huyo lilikwama.


 
Tangu aondoke kocha Didier Gomes, Wawa amekuwa na wakati mgumu kucheza mara kwa mara kama ilivyokuwa misimu miwili iliyopita na pia mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu sambamba na nyota wengine 12.

Katika nafasi ya beki wa kati anayocheza, Joash Onyango na Henock Inonga wanacheza mara kwa mara. Miongoni mwa sababu zinazotajwa Wawa kuachwa ni kushindwa kucheza kikosi cha kwanza, umri mkubwa, kufanya makosa ya kiulinzi mara kwa mara, kutocheza kwa ubora kama wakati aliotua hapa nchini.

Kuondoka kwake kutafungua mlango beki wa kigeni kutua Msimbazi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad