Zelensky Awalaumu Umoja wa Ulaya "Mlichelewa kuzuia uvamizi wa Urusi"



Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alitoa hotuba ya usiku wa manane kwenye mkutano wa kilele wa Baraza la Ulaya mjini Brussels.

Alielezea uharibifu na mauaji ya Urusi kwa nchi yake, na akashukuru Ulaya kwa kuungana katika msaada wao kwa Ukraine.

Kisha, kwa mtindo wake wa kusema mambo moja kwa moja, aliwaambia viongozi wa Ulaya kwamba walikuwa wamechelewa sana kuizuia Urusi.


"Mmeweka vikwazo, tunashukuru. Hizi ni hatua zenye nguvu.

"Lakini ilikuwa ni kuchelewa kidogo ... kulikuwa na nafasi," alisema, akiongeza kuwa kama kungekuwa na vikwazo vya kuzuia labda Urusi isingeingia vitani.

Pia aliashiria bomba la gesi la Nord Stream 2, ambapo alipendekeza ikiwa lingezuiwa mapema, "Urusi isingeleta shida ya gesi".

Zelensky kisha akaomba mataifa jirani kuidhinisha ombi la Ukraine la kujiunga na EU.

"Hapa nawauliza - msichelewe."

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad