Zelensky: Mazungumzo yakifeli ni vita ya tatu ya dunia



Siku ya jumapili, Rais wa Ukraine Zelensky akizungmza na na shirika la habari la CNN alisema yuko tayari kuzungumza moja kwa moja na Rais wa Urusi  Mhe Vladimir Putin, kwakua anaamini kuwa mazungumzo ndiyo njia pekee ya kumaliza mgogoro.

“Nadhani tunapaswa kutumia muundo wowote, nafasi yoyote ili kuwa na uwezekano  wa kufanya mazungumzo”Alisema  “Kushindwa kufanikisha mazungumzo ya kumaliza uvamizi wa Urusi kutamaanisha vita vya tatu vya dunia” aliongezea.

Zelensky anaamini pia kwamba kama nchi yake ingekuwa mwanachama wa NATO, asingweza kuvamiwa na akatumia fursa hiyo kuwaomba awe mwanachama ili kunusuru raia wake wanaouwawa na majeshi ya Urusi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad