Zuchu "Ni Tanzania pekee ndiyo tuna industry ya muziki iliyojaa mzaha na vichekesho"



MUZIKI wa Tanzania umechukua mwelekeo mpya, lengo likiwa ni kuupeleka mbali zaidi huko duniani. Jitihada nyingi zimekuwa zikifanywa kuhakikisha muziki wa Bongo Fleva unafika mbali zaidi. Lakini katikati ya jitihada hizo, Zuchu; ni malkia mpya wa muziki nchini Tanzania ambaye analalamika kwamba kuna mchezo mchafu unaendelea kwenye tasnia hiyo ya muziki nchini Tanzania.

Hii ni baada ya Chama cha Muziki Tanzania (TMA) kutaja majina ya wasanii walioteuliwa kuwania tuzo mbalimbali huku kukiwa hakuna jina la msanii hata mmoja ambaye yupo chini ya Lebo ya WCB Wasafi inayomilikiwa na Diamond Platnumz.

Hata hivyo, Zuchu amewashukuru mashabiki wake akiwaambia wahusika wanajua ukweli ndiyo maana hakuna jina lake. Zuchu amesema; “Ni Tanzania pekee ndiyo tuna industry ya muziki iliyojaa mzaha na vichekesho ndani yake, inatia aibu maana hii mitandao tunaitumia kujichoresha kwa michezo ya kitoto tunayocheza.

“Mimi nawashukuru Watanzania walio wengi bila hata kushurutishwa mnajua mbivu na mbichi, mnatupambania sana wasanii wenu, that’s the only thing kinanipa nguvu kwa sababu ninyi ndiyo mnatuweka tulipo.

“But as for the industry yetu kwa jumla inatia huruma na hasira, imagine hata sehemu ya kufanyia shoo za maana hatuna, haki zetu ndizo hizo zinachezewa sandakalawe. “Tumefanywa daraja la watu wasiojali tasnia kupata umaarufu tu wa kupata kipato.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad