Web

Afariki baada ya kupigwa na mtungi wa gesi kichwani



Simanjiro. Mpishi wa hoteli kwenye machimbo ya madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro, Mkoani Manyara, Mussa Patrick (22) amefariki dunia kwa kupigwa na mtungi wa gesi kichwani.

Akizungumza na Mwananchi Digital Kaimu kamanda wa Polisi mkoani humo, Limited Mhongole amesema tukio hilo limetokea Machi 29 katika eneo la Soko la Dodoma kwenye machimbo ya Tanzanite Kitalu B.

Amesema marehemu ameuawa akiwa amelala baada ya mwenzake baada ya mwenzake kumpiga na mtungi wa gesi kichwani.

Kamanda Mhongole amesema mtumiwa Nelson Migalo (18) anatafutwa baada ya kutoroka


 
“Kulitokea ugomvi baada ya marehemu kumwambia mtuhumiwa aache kupiga muziki wakati anasali saa 4:00 usiku, waliamuliwa ilipofika saa 8:00 usiku mtuhumiwa alienda kufanya unyama huo” amesema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad