Ali Kamwe "Simba wametusaidia sana kutengeneza 'STANDARD' ya Tanzania kwenye michuano ya Kimataifa


Ndani ya Miaka mitano, Robo Fainali Tatu za Michuano ya CAF? Asante Simba

Haya sio mafanikio yao pekeyao.. Ni Jambo la kujivunia kwa kila Mtanzania. Kwanini?

Simba wametusaidia sana kutengeneza 'STANDARD' ya Tanzania kwenye michuano ya Kimataifa

Ni Simba waliofanya Watanzania Tuone kucheza Hatua ya Makundi ya CAF kama jambo la kawaida

Usipocheza GROUP STAGE, inatafsirika kama kufeli

Ni tofauti kidogo na ilivyokuwa miaka ya nyuma kidogo.. Timu zetu hata kufuzu hatua ya pili ilikuwa Stori kubwa ya kujivunia!

'Perfomance' ya Simba itatusaidia kupandisha Standard ya Klabu zetu kwenye michuano ya CAF

Mashabiki wa Yanga watatamani kuiona Timu yao kwenye HATUA YA MAKUNDI.

AZAM pia.. Iwe Namungo au KMC.. Target namba moja sasa ni kucheza Makundi na si vinginevyo.

Simba wameshatuonyesha kuwa inawezekana. Sio suala la kupiga ramli tena.

Ni wakati sasa Dunia kuanza kuitazama TANZANIA kama ONE OF THE GIANTS wa Afrika kwenye ngazi ya Klabu!

Tusikubali tena kurudi nyuma. Kipimo cha Ubora Tumeshakipata.

ASANTE SIMBA 🙏

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad