Alikamwe "Mambo 10 nilioyaona SIMBA vs GENDARMERIE Mtu Akupigwa 4



1: THIS IS SIMBAAA..🦁 WOW! .. JUST WOW.. KIBABE, KIKUBWA Mnyama Simba anatimba ROBO FAINALI ya Kombe la CAF..

2: Sahau kuhusu Heshima.. Sahau kuhusu Rekodi.. Muda huu Akaunti ya Benki ya Simba inasubiri Bonus ya Dola za Kimarekani 350,000 [ Zaidi ya Milioni 800 za Kitanzania].. Klabu kubwa yenye Malengo makubwa🙌

3: Tumezishuhudia Simba 2 tofauti ndani ya Dakika 90! Kwanini? Kipindi cha kwanza, Simba iliongozwa na presha kubwa kwenye vifua vya wachezaji... Kipindi cha pili, Timu ikaongozwa kwa akili kubwa kichwani. Mabao 4 yakapatikana!

4: Kwanini presha? Huu ulikuwa mchezo wa maamuzi. Ni kama kila mchezaji alipania kufanya jambo kwa ajili ya Simba. Hii ikazaa 'ubinafsi' na kukosa utulivu kwenye eneo la mwisho. Na hii ndio sababu walipiga mashuti 11 lakini ON TARGET ilikuwa moja Tu.

5: Nafikiri kuna kazi kubwa ilifanyika vyumbani wakati wa mapumziko. Saikolojia za wachezaji ilirudi mahala pake. Uchoyo ukapungua kwenye eneo la mwisho na kila mmoja akarudi kucheza kwa ajili ya Timu👏

6: Gendarmerie walikabia kwenye Mid Block Lakini hawakuwa compact kabisa. Situation za 1v1 zilikuwa nyingi kwa Morrison. Tactically Pablo alikwenda uwanjani na mpango sahihi.. Kama utulivu ungepatikana mapema, mechi ingeweza kumalizika mapema

7: MORRISON! WHAT A PLAYER! Katika matukio makubwa anakupa Thamani yake kiwanjani. Mikimbio yake, Ubunifu wake, uwezo wake wa kuona pasi sahihi kwenye eneo la mwisho uliwapa wakati mgumu sana mabeki wa Gendarmerie

8: Yule Adebayor Mtu wa maana sana🙌 Simba wakitaka kujua ubora wake hawatakiwi kwenda YouTube.. Wamuulize tu ONYANGO! Mikimbio sahihi, uwezo wa kupiga.. What A Player!

9: Nilipenda sana Fighting Spirit ya wachezaji wa Simba! Wanastahili pongezi kubwa. Kuna Faida pia wako nayo kwenye uzoefu wa mechi za Kimataifa! Hata pale bahati ilipoonekana haiko upande wao bado walitulia sana!

10: Hongera pia kwa mashabiki wa Simba👏 Mchango wao umeonekana! VIBE LA MAANA SANA na Vitochi tumeviona😃

Nb: Hakuna namna.. Tumshukuru Rais kwa Simba.. 😃

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad