Aliyejenga nyumba ya milioni 300 Ngorongoro akubali kuhama



MAKAMU Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha, Foibe Lukumay (70), ni miongoni mwa watu waliojenga nyumba ndani ya eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) yenye thamani ya Sh.milioni 300 amekubali kuhama kwa hiari.

Foibe Lukumay, Mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Enduleni, Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha, akiwa nje ya nyumba yake anayodai kuijenga kwa Sh.milioni 300. PICHA:GODFREY MUSHI
Foibe, mama wa watoto 12, amesema: "Nimekaa nikafikiria nikazungumza na watoto wangu wote kwa mtandao kwa njia ya zoom, tukakubalina hakuna haja ya kusumbuana na serikali.

"Wakaniambia mama hama tu, na tena wenyewe ndio walioniandikia barua ya kuomba kuhama kwa hiari na nifidiwe nyumba zangu nilizojenga Kijiji cha Enduleni pamoja na nyingine zilizopo huko mbele. 

"Nilipeleka barua hiyo kwa Kamishna Mkuu wa Uhifadhi wa NCAA na tayari wamekuja kufanya uthamini wa nyumba yangu na kuipa namba.

"Ninachosubiri ni kuambiwa siku ya kuondoka, na kwa kweli watu waachwe wasirubuniwe na baadhi ya watu wakiwashawishi wasihame."
Foibe ambaye ni Mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Enduleni, amedai kuwa ujenzi wa makazi ndani ya hifadhi hiyo unachagizwa na gharama kubwa zinazotokana na kuagiza malighafi ya ujenzi katika wilaya jirani ya Karatu iliyopo umbali wa zaidi ya kilomita 62.3.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad