Baada ya Kutoa Onyo, Urusi Yasogeza Zana za Kivita Kwenye Mpaka Wake na Finland




Zana za Kivita za Urusi zinaelekea mpakani mwa nchi hiyo na Finland
HIVI karibuni Urusi ilitoa onyo juu ya mataifa mawili ya Finland na Sweden kuhusu mpango wao wa kujiunga na NATO lakini kumekuwa na harakati mbalimbali ambazo zinaashiria Finland na Sweden kupuuzia onyo hilo.

Huku vita baina yake na Ukraine ikiwa inaendelea Urusi imetuma vikosi vyenye zana nzito za kivita kuelekea katika eneo la Finnish ambalo ndiyo ulipo mpaka wa Finland na Urusi.

Waziri Mkuu wa Finland Sana Marin amesema anategemea serikali yake kufikia majira ya kiangazi mwaka huu itakuwa imemaliza majadiliano kuhusu uwezekano wa kuomba uanachama wa NATO.

Picha za video zimeonesha msafara wa majeshi ya Urusi ukiwa na mfumo wa makombora ukielekea kaskazini mwa Urusi ambako ndiko inakopakana na nchi ya Finland.


 

                           Urusi imeamua kupeleka zana zake za kivita kwenye mpaka na nchi ya Finland
Makombora yaliyobebwa yanasadikika kuwa ni aina ya K-300P Bastion yanayotumika kulipua meli pamoja na ndege za kivita.

Hivi karibuni ulifanyika utafiti chini Finland kuhusu hali ya usalama nchini humo ambapo asilimia 84 ilionesha Urusi ndiyo taifa linalotishia usalama wan chi hiyo.

Msemaji wa Urusi Dmitry Peskov ameonya kuwa hatua ya Finland kujiunga na NATO haitakuwa na faida yoyote kwa usalama wa Ulaya, naye Vladimir Dzhabarov alienda mbali Zaidi na kusema kuwa Finland kujiunga na NATO ni tafsiri ya kusambaratika kwa nchi hiyo.


“Tumekuwa tukirudia kuongea mara kwa mara kuwa ushirikiano wao ni njia ya kusababisha machafuko na hakutaleta Amani ndani ya nchi za Ulaya.” Alisema Peskov.

Jana NATO ilitangaza kuwa meli za kivita kutoka mataifa mbalimbali yanayounda Umoja wa Kujihami zikiongozwa na jeshi la Uholanzi zitafanya ukaguzi na ulinzi katika maeneo ya pwani ya bahari ya Baltic ambayo inaunganisha nchi wanachamama wa NATO zikiwemo Poland na Estonia lengo likiwa ni kuimarisha ulinzi katika maeneo hayo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad