Baada ya Mugalu Kuharibu, Simba Yapata Mtambo wa Mabao Sauz



UNAAMBIWA kosa la kupigwa kadi nyekundu kwa mshambuliaji Chris Mugalu limemfanya Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco kuwaomba viongozi wake kuhakikisha wanamshawishi mmoja wa mastraika wa Orlando Pirates ya Afrika Kusini, Tshegofatso Mabasa kumsajili kwa ajili ya msimu ujao.

 

Mabasa alijiunga na Orlando Pirates Julai Mosi, 2019, akitokea katika Klabu ya Bloem Celtic ya nchini humo, baada ya kuonyesha uwezo mkubwa katika upande wa ufungaji, mbali na hivyo, Mabasa msimu huu hadi sasa amefunga mabao mawili na asisti mbili katika mechi 13 za Ligi Kuu ya Afrika Kusini.

 

Mugalu aliifanya Simba icheze pungufu kwa dakika 32 kwenye mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Orlando Pirates, alipata kadi dakika ya 58 na dakika mbili mbele Orlando wakapata bao, hivyo kwenda kwenye penalti na Simba wakatolewa kwa mikwaju 4-3.

 

Chanzo chetu kutoka Simba, kimethibitisha kuwa, Kocha Pablo amevutiwa na uchezaji wa Mabasa, hivyo akawashauri mabosi wa Simba kufanya mazungumzo naye ili kuangalia uwezekano wa kumsajili kwa ajili ya msimu ujao.

 

“Ninachokijua mimi hapa ni kuwa, baada ya mchezo wetu wa leo (juzi Jumapili), kuna mpango wa kocha Pablo kuzungumza na uongozi kama wataweza kumshawishi yule Mabasa wa Orlando ili wamsajili kwa ajili ya kuwa mbadala wa Mugalu.


Mshambuliaji wa Klabu ya Simba Chris Kope Mugalu

“Kiukweli kocha Pablo nadhani kuna kitu cha zaida amekiona kwa huyu Mabasa kwani pamoja na kuwepo kwa straika kama Kwame Peprah, ila yeye naona ameonyesha nia kubwa ya kumtaka Mabasa, jambo ambalo tayari ameahidi kulifikisha kwa uongozi,” kilisema chanzo hicho.

 

Championi Jumatano lilimtafuta Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally ili azungumzia ishu hiyo ambapo alisema: “Kuhusiana na Mabasa kiukweli sina taarifa rasmi ila kama kuna taarifa kama hiyo basi itakuwa kuna kitu kocha mwenyewe amekiona kwa mchezaji huyo.

 

“Kikubwa ninachoweza kukwambia ni kuwa, hatujaanza kutaja majina ya usajili ila kwa ufupi tu ni kwamba Orlando ina wachezaji wengi sana wazuri na wenye uwezo wa kusajili Simba na kubadilisha kabisa hali ya timu yetu.”

 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad