Bashungwa Awakingia Kifua Dereva Bajaji Walemavu


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Innocent Bashungwa, ametengua katazo lililotolewa na Halmashauri ya jiji la Dar es salaam kuhusu dereva wa Bodaboda kuingia Mjini katika Jiji la Dar es Salaam.

Bashungwa amefikia uamuzi huo baada ya madereva Bodaboda Pamoja na Bajaji wakimwemo wenye ulemavu kuandamana mpaka kwenye ofisi za mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla wakitaka agizo hilo lisitishwe.

Madereva hao walisema kuwa Tamko hilo haliendani na makubaliano waliyoyafanya katika kikao cha Pamoja yaliyohusu waendesha bajaji wenye ulemavu na waendesha bodaboda wasio na ulemavu.

Miongoni mwa Makubaliano waliyoyafanya ni Pamoja na Bajaji za watu wenye ulemavu kuruhusiwa kuingia katikati ya mji, na kuegesha kwenye vituo vitatu vilivyopangwa, bajaji za wasio na ulemavu kutoruhusiwa kuingia mjini kabisa, bodaboda zilizosajiliwa na kukidhi vigezo kuruhusiwa kuegesha kwenye vituo saba katikati ya mji na bodaboda zisizokuwa na vigezo wala vibali kuruhusiwa kuingia mjini kwa kigezo cha kushusha abiria na kuondoka

Katika jitihada za kutuliza maandamano hayo ndipo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala alipompigia simu Waziri Bashungwa na kumueleza makubaliano hayo na hali ilivyokua kwa wakati huo ndipo Bashungwa aliporidhia kutengua katazo hilo na kuwasihi kuendelea na utaratibu uliokua umewekwa hapo awali.

Hata hivyo Waziri Bashungwa amewataka wahusika wote kukaa Pamoja na kupata nafasi ya kutafakari Zaidi namna bora ya kushughulika na jambo hilo.

Katazo hilo lilitolewa April 20 na halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad