Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi amesema anachojua Ndugai hayupo Bungeni na inawezekana atakuwa Jimboni kwake kwa mujibu wa Kanuni na Taratibu za Bunge lakini hana barua rasmi ya kutokuwepo kwake katika Mkutano wa Bunge la Bajeti unaoendelea tangu kuanza Aprili 5, 2022.