Dar Mpya waonywa habari za Bunge



Spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson Mwansasu amevionya vyombo vya Habari na wahariri wa madawati ya Habari juu ya uandishi wa Habari zisizokuwa na ukweli hasa zinazohusu Bunge na wabunge wote.

Akizungumza jana Bungeni Jijini Dodoma wakati akifunga Kikao cha sita, mkutano wa 7 bunge la 12, Dkt. Tulia amesema Waandishi wa Habari wamepewa ruhusa ya kuingia Bungeni na wamepewa nafasi ya kufanya mahojiano na mbunge yeyote ambae kuna jambo wanahitaji ufafanuzi hivyo hawapaswi kuandika mambo ya kutunga.

Spika Dkt Tulia, amesema kuwa Bunge halihitaji kufanya kazi kwa ubaya na waandishi wa habari kwa kuwa wao wanawasaidia kutoa taarifa za mambo yayayotokea na kwa manufaa ya majimbo yao na hawataki ifike wakati ambao baadhi ya vyombo vitafungiwa kujihusisha na masuala ya Bunge kwa kukiuka kanuni.

“Sasa tuko katika kipindi ambacho yatu wasituvute sana alafu wakaanza kuitwa hapa maana mamlaka hayo tunayo, Vyombo vya habari tupo tayari kuwapa ushirikiano na tutaendelea kuwapa ushirikiano na tarifa zote mnazozitaka tunazo na tutawapa msiandike taarifa za upotoshaji,” alisema Dkt. Tulia.


Spika Tulia ameongeza kuwa waandishi ambao wanaruhusiwa kuingia Bungeni wanazo nafasi za kuzungumza na wabunge, wasiwe na tabia za kupotosha akitaja chombo cha habari cha Dar Mpya kama mfano wa vyombo vilivyopotosha jamii kuhusu habari za Bunge.

“Dar Mpya Blog, nawaonya sana, msipotoshe umma. Niwaonye hawa Dar Mpya Blog kufuata utaratibu na wasifanye mambo kama haya na niwaombe viongozi wanaoongoza vyombo vya habari wafuate utaratibu na sisi tumefungua Milango wazi ili kuleta ushirikiano na tutumie njia hizo kupata taarifa rasmi.” Ameongeza Dkt. Tulia.

Aidha Spika Tulia ametoa wito kwa vyombo vya habari vyote kama wanataka taarifa zinazohusu bunge na wabunge wote zinapatikana ndani ya ofisi ya Bunge hivyo wajiridhishe kwa kupitia huko.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad