DJ Khaled ataungana na mastaa wengine wakubwa duniani waliopewa heshima ya kutunukiwa nyota kwenye Hollywood Walk of Fame. Kwa mujibu wa mtandao wa Variety, #Khaled atatunukiwa nyota hiyo April 11, mwaka huu.
@djkhaled ambaye jina lake halisi ni Daverneius Jaimes Khaled amewahi kushinda tuzo za Grammy mara moja, ni mwandishi wa nyimbo na ni mtayarishaji wa muziki. Ametajwa kuwa atatunukiwa nyota hiyo hii ni kutokana na mchango wake mkubwa kwenye tasnia ya muziki kwa zaidi ya miaka 18.
Fahamu, Hollywood Walk of Fame ni eneo la kutembea kwa miguu kando kando ya majengo katika eneo la Hollywood ambapo nyota za watu waliofanya vyema kwenye upande wa burudani zimewekwa. Walengwa ni wanamuziki, waigizaji, waelekezi wa filamu, watayarishaji wa muziki na filamu na makundi ya waigizaji.