Dkt. Slaa afichua siri, Samwel Sitta alitaka kuhamia CHADEMA



Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA na hivi karibuni amekuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden mpaka anapostaafu Dkt. Wilbroad Peter Slaa, amesema katika Uchaguzi wa mwaka 2010 CHADEMA walimuandaa Samwel Sitta kuwa mgombea mkuu wa upinzani.

Dkt. Slaa amesema hayo katika mahojiano maalumu na Dar24 alipotembelewa nyumbani kwake na kuzungumzia maisha yake kwa ujumla, Siasa alizozifanya pamoja na masuala ya kijamii.

Amesema kuwa yeye hakuwa amejiandaa kugombea na wala hakuwa na mpango wa kuwa Rais katika Maisha yake ingawa mipango ya Chama chake iliposhindikana ndipo akateuliwa kuwa mgombea.

“Sisi CHADEMA wakati huo mwaka 2010 tulianza kuandaa mgombea wetu tangu Januari, na mimi nilipewa kazi ya kumuandaa mgombea wa Urais, wakati huo nikiwa Katibu Mkuu na pia nikiwa kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na nilifanya kazi zangu kwa uaminifu na uadilifu mkubwa bila kujiwekea kuwa nafasi hiyo nitaenda kuichukua mimi,” alisema


 
“Alikua Muheshimiwa Samweli Sitta awe mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA na mipango yote ilikamilika bahati mbaya mipango hiyo ilifeli dakika ya mwisho mwezi Julai karibia na kipindi cha kupiga kura ya kupitisha bajeti ya 2010/2011 ndio mipango ilishindikana. Sasa mimi nilishtukishwa na kamati kuu kuwa baada ya hapo Mgombea wetu wa CHADEMA atakua Dkt. Slaa, nilishtuka, niliugua na nililala siku mbili mbele niliumwa.”

Akiendelea kufafanua zaidi kuhusiana na suala hilo la kuwa Rais, Dkt. Slaa amesema kuwa aliipokea na kujiandaa kwa kuwa alikua amepitia Ubunge kwa miaka 15 hivyo siasa aliziweza ingawa hakuwahi kuwa na tamaa ya kutaka kuwa Rais katika harakati zake siasa.

Hata hivyo Dkt. Slaa amesema kwa sasa hana shughuli anayojishughulisha nayo ambapo anapumzika, na kutafakari masuala ambayo ameyapitia katika maisha yake.


“Kama nilivyosema tangu naachana na CHADEMA, mimi sasa nipo huru sifungamani na chama chochote, nipo huru, na mimi sasa nina Furaha na nipo huru kusema kile ambacho ninatyaka kusema kuhusu nchi yangu,” amesema Dkt. Slaa.

“Kutumikia Taifa ni Mpaka pale unapoingia Kaburini hivyo kama kutatoea nafasi ambayo itanitaka kutumikia taifa bila kujihusisha na chama niko tayari na umri wangu haunizuii, ingawa mimi tangu nilipojitoa CHADEMA nilifamua kujitoa kwenye siasa za vyama, na kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huwezi kuwa kiongozi yoyote kama huna chama cha siada. Lakini hiyo kitu sasa Muda wake umeisha kwangu,” aliongeza Dkt. Slaa.

Dkt. Slaa ametolea ufafanuzi suala ambale limekua likizungumzwa na watu wengi kuhusiana na yeye kupata ubalozi kupitia Tiketi ya CCM.

“Watu wengi mpaka leo wanaamini kuwa mimi nilihongwa kuingia kwenye ubalozi kwa kupitia Chama cha Mapinduzi, lakini mimi sikuhongwa, wala sija Compromise huo uamuzi wangu wa kutoshiriki Siasa za vyama. Na bahati nzuri hatya Rais wangu aliyeniteua nilimwambia usije ukaniambia nitekeleze ilani ya Chama fulani, nilimwambia nitatekeleza Ilani ya Nchi ambayo inaongozwa na Chama kilichoshinda,” Dkt. Slaa.


 
Pamoja na maelezo hayo Dkt. Slaa ameandika kitabu ambacho bado hakijasambaa sana kinachoitwa ‘Nyuma ya Pazia: CHADEMA livyosalitiwa mwaka 2015’, lakini amesema kwa sasa haoni tatizo kwa Serikali ya sasa kwa kuwa inaendelea kufuata nyayo za kufungua Dunia na kusaidia wanyonge.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad