Fifa Yakana Mpango wa Kuongeza Dakika za Mpira Kutoka 90 Kwenda 100 Kombe la Dunia


Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA lakana mpango wa kuongeza dakika kutoka zile za awali 90 hadi 100 kwenye michezo ya kombe la dunia ambalo linakwenda kufanyika nchini Qatar mwaka huu.

Taarifa za kuwa shirikisho hilo limepanga kufanya mabadiliko zilianza kushamiri jana Jumatano, kuwa FIFA wamepanga kufanya mabadiliko ya dakika kwenye michezo ya kombe la dunia mwaka huu.

Gazeti la Corriere dello Sport lilitoa taarifa za kudai kuwa wazo hilo lilitoka moja kwa moja kwa rais wa shirikisho hilo Gianni Infantino, lakini wazo lolote linalotolewa na shirikisho hilo linahitaji kupata kibali cha uthibitisho kutoka IFAB.

Saa chache baada ya tetesi hizo kuzagaa kuhusu kuongeza dakika za mchezo, FIFA wameamua kulioandoa kabla hata kulipeka kwenye bodi ya IFAB kwa ajiri ya kibali cha uthibitisho.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad