Gambo Alia Soko la Madini ya Tanzanite Kuhamishiwa Mirerani



Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo (CCM) ameeleza hasara iliyopatikana kwa uamuzi wa Serikali kuhamishia soko la madini ya Tanzanite kutoka Arusha mjini na kuhamishia katika mji wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Akichangia hoja katika bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara zake leo Jumatatu tarehe 11 Aprili 2022, Gambo amesema wakati madini mengine yote yanauzwa katika soko la Arusha ni Tanzanite pekee ndiyo iimepigwa marufuku.

Amesema tangu kahamishwa kwa soko hilo uzalishaji wa madini hayo umepungua sambamba na kupungua kwa mapato ya Serikali.

“Hatua ya kubadilisha kanuni imeipatia Julai hadi Desemba 2019 serikali iliweza kareti 76,000 na kodi milioni 487 huku kwenye Tanzanite ambayo haijakatwa Serikali ikipa kodi ya Sh 1.3 bilioni.


Amesema mwaka 2020 ilizalishwa karate 85,000 na kodi ya Sh 332 milioni lakini nak kwenye tanzanite ambayo haijaongezewa thamani ilipatikana kodi ya Sh 1.1 bilioni.

“Baada ya kuhamishiwa Mirerani ukiangalia kwa kipindi kilekile cha Julai hadi Januari Serikali imepata kodi kiasi cha Sh 339 milioni kutoka Sh 1.3 bilioni na kwa upande wa karati tumezalisha 15,000 kutoka 85,000.

“Kwahiyo unaona kabisa maamuzi haya yamekwenda kuitia hasara serikali ,” amesema Gambo.

Ameongeza kuwa wakati soko likiwa Arusha kulikuwa na wauzaji 103 lakini Mirerani kuna wafanyabiashara 48 pekee.

“Lakini kuna ajira zaidi ya 413 zimepotea na madalali kutoka 2500 mpaka 300 ambao wamekosa ajira,” amesema Gambo.

Amesema Serikali imepata hasara yaSh 128 milioni kwa kukosa kodi ya pango katika majengo ambayo yalikuwa yanatumika na wafanyabiashara kama masoko.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad