GIFT STANFORD au Gigy Money ni mwanamama wa Bongo Fleva ambaye anasema kuwa, watu wasichokijua ni sawa na usiku wa giza hivyo waache kuongea mambo wasiyokuwa na uhakika nayo.
Akizungumza na #SHOWBIZ, Gigy anasema kuwa, kumekuwa na maneno mengi baada ya mzazi mwenzie MOJ kuoa, jambo ambalo halimuumizi hata kudogo.
“Mimi siumizwi na mzazi mwenzangu (MOJ) kuoa kwa sababu tulishamalizana muda mrefu sana, isitoshe nipo kwenye uhusiano na mwanaume ninayempenda sana na yeye ananipenda sana, ndiyo maana nasema usichokijua ni kama usiku wa giza,” anasema Gigy ambaye amezaa mtoto wa kike na MOJ.