Harsi Said "Tutachukua Ligi Kuu na na Kombe la Shirikisho"


Uongozi wa Young Africans umewataka wachezaji kutoridhika kwani bado safari yao ni ndefu ya kuhakikisha wanafikia malengo waliyojiwekea katika Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’, msimu huu 2021/22.


Young Africans inaongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa kufikisha alama 51, baada ya kucheza michezo 19, huku ikitinga hatua ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ na keshokutwa itacheza dhidi ya Geita Gold Jijini Dar es salaam.


Mjumbe wa Kamati ya Usajili ya Klabu hiyo Hersi Said amesema hawajapoteza hadi sasa na malengo yao kuendelea kupata matokeo, ana imani kwa hali waliyofikia bado wapo kwenye safari ndefu zaidi ya walipotoka.


Amesema malengo yao makubwa ni kihakikisha msimu huu wanatwaa ubingwa wa ligi hiyo ambao wameukosa kwa misimu mitano mfululizo pamoja na taji la Kombe la Shirikisho ‘ASFC’.


 “Tunashukuru tumefanikiwa kufanya vizuri katika michezo 19 hatujapoteza, wachezaji hawatakiwi kuridhika haraka kwa sababu tunapokwenda ni ni kugumu na tuko katika safari ndefu ya kufikia malengo yetu,” amesema Hersi.


Young Africans itakuwa nyumbani ikiwakaribisha Geita Gold katika mchezo huo utakaopigwa, Aprili 10 mwaka huu katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad