Hatimaye Oscar Watoa Adhabu Kwa Will Smith Kumpiga Kofi Chris Rock, Miaka 10 Yamuhusu


Mwigizaji Will Smith hatoruhusiwa kuhudhuria Tuzo za Oscar kwa miaka 10 kutoka sasa ikiwa ni adhabu baada ya kumpiga kibao Mchekeshaji Chris Rock jukwaani wakati wa Tuzo hizo mwaka huu.

Bodi ya Tuzo hizo imetangaza kwamba kwa miaka hiyo 10 kuanzia Aprili 8, 2022, Smith hatoruhusiwa kuhudhuria hafla au programu zozote za Academy, yeye binafsi au hata kwa mtandao.

Baada ya marufuku hii ya miaka 10 Will Smith ameonesha kukubali adhabu aliyopewa kwa kuiambia CNN kwamba "ninakubali na kuheshimu uamuzi wa Academy" ambapo uamuzi huu umekuja kufuatia mijadala mingi baada ya kumpiga Chris kofi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad