Afrika Kusini imetangaza ukomo wa sheria za kukabiliana na Covid, miaka miwili baada ya sheria hizo kuwekwa kote nchini humo.
Katika hotuba yake iliyotangazwa kwa televisheni, Rais Cyril Ramaphosa alisema kuwa hali ya janga ya taifa itamalizika usiku saa sita Jumatatu.
Barakoa hatahivy zitaendelea kuvaliwa katika kumbi zenye mikusanyiko ya watu kwa kipindi cha mwezi mwingine mmoja.
Alisema eingawa janga bado halijaisha, anaamini kwamba kuna siku njema zijazo mbeleni.
Bw Ramaphosa alisema ni muhimu kuinua uchumi na kubuni ajira
Afrika kusini imerekodi visa zaidi vya virusi vya corona kuliko nchi nyingine yoyote ile ya Afrika, ikiwa na takriban robo tatu ya maambukizi yote barani Afrika.
Ilirekodi vifo rasmi 100,000 vilivyotokana na corona.