Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ limemtaja Mwamuzi Bernard Camille kutoka Visiwa vya Shelisheli kuwa msimamizi wa Sheria 17 za mchezo wa Mkondo wa Pili Hatua ya Robo Fainali, Kombe la Shirikisho.
Simba SC itakua mgeni wa Orlando Pirates Jumapili (April 24), katika Uwanja wa Orlando nchini Afrika Kusini, huku ikiwa na mtaji wa bao moja kwa sifuri.
CAF pia imewataja waamuzi wasaidizi katika mchezo huo ambao ni James Emile FredrickLast (Visiwa vya Shelisheli) na Lionel Hasinjarasoa Last Andrianantenaina (Madagascar).
Mwamuzi wa akiba atakua Hélder de Carvalho MartinsLast kutoka Angola.
Mchezo wa Mkondo wa Pili kati ya Simba SC dhidi ya Orlando Pirates umepangwa kuanza mishale ya saa kumi na mbili kwa saa za Afrika Kusini, saa moja usiku kwa saa za Tanzania.
Simba SC italazimika kulinda ushindi wake wa 1-0, ama kusaka ushindi zaidi katika mchezo wa Mkondo wa pili ugenini Afrika Kusini siku ya Jumapili (April 24), ili kupata tiketi ya kutinga Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Kwa upande wa Orlando Pirates italazimika kusaka ushindi wa mabao mawili kwa sifuri na kuelendelea, ili kujihakikishia nafasi ya kucheza Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika.