Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, umenyetisha kuwa mwanamama Jennifer Lopez na Ben Affleck wanaelekea kufunga ndoa, hii ni baada ya J Lo kuonekana amevaa pete kubwa ya uchumba yenye madini ya Almasi kwenye kidole chake na kuificha baada ya kuona mapaparazi wa TMZ.
Ndoa hiyo ambayo inatajwa, inaenda kuwa ya nne kwa J Lo na ya pili kwa Ben Affleck.