Jux apongeza Serikali kwa tuzo za Muziki



Mkali wa R&B kutoka katika tasnia ya muziki wa Bongo fleva Juma Jux amekuwa mmoja wa wasanii walioonesha heshima na kufurahishwa na ujio wa tuzo za muziki Tanzania kwa kutoa shukurani na pongezi kwa timu nzima ya waandaaji wa tuzo hizo ambao ni Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kupitia Baraza la Sanaa la Taifa.


Katika mtandao wake wa Instagram, Jux ameweka wazi kuwa kurejea kwa tuzo hizo kutarejesha heshima ya muziki wa Tanzania na kuwa chachu ya kuongeza ushindani na ari kwa wasanii kupambana kufanya kazi zenye ubora na viwango stahiki.


“Kuelekea kwenye kilele cha Tuzo za Muziki za hapa nyumbani, napenda kutoa shukrani na pongezi zangu za dhati kwa wote walioshiriki kwenye uandaaji wa tuzo hizi zenye lengo la kupongeza uwezo na vipaji vya wasanii wengi hapa nchini, hongera sana BASATA kwa kurudisha heshima ya wasanii na kutimiza ndoto za wasanii wengi kutambulika kwa vipaji na uwezo wao,”


Nawashukuru watanzania wote kwa kuendelea kuni-support kwenye shughuli zangu za kimuziki na biashara, na kwa wakati huu nawashukuru kwa kunipigia kura kwenye vipengele Saba (7) nilivyotokea kwenye TMA Tuoneshe ushirikiano kwa kuzifuatilia tuzo hizi kwa ukaribu.” Aliandika Jux.


Tuzo za muziki 2021 zinatarajiwa kutolewa usiku wa leo April 2, 2022 katika Kituo cha mikutano cha Mwalimu Julia Nyerere jijini Dar es salaam.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad