Kajala Masanja "Nilipovunja Sijengi"


Harmonize amekuwa akifanya kila liwezekanalo kumshawishi ex-wake, mwigizaji Kajala Masanja au Mama Paul amrudie.

Katika juhudi hizo, Harmonize au Konde Boy Mjeshi amekuwa akimuandikia mwigiaji huyo jumbe mbalimbali za kuomba msamaha na hata kuweka bango la picha yao pale Kinondoni-Manyanya jijini Dar.

Harmonize anakiri kwamba amekuwa akipitia kipindi kigumu tangu alipokosana na Kajala mwaka jana na hadi kufikia hatua ya kuathirika kisaikolojia.

“Nimekuwa sawa, nimekuwa nikitengeneza muziki, lakini kuna wakati nilisema sasa imezidi. Mimi sina raha. Mimi ni Harmonize, naweza kutumia umaarufu wangu kupata mwanamke mrembo zaidi kuliko, nimejaribu na kila mtu anajua.

“Lakini ilifika wakati nikasema namtaka yeye tena. Nataka kila mtu ajue hali ambayo nimekuwa nikipitia. Imekuwa mbaya, siku tatu sikutoka nje, nilikuwa nakunywa dawa tu. Imekuwa tatizo kwangu.

Ni kitu ambacho nahisi ndani yangu," anasema Harmonize.
Baada ya ukimya wa muda mrefu kuhusu ishu hiyo, hatimaye Kajala amejibu kimafumbo.
Katika kile kilichoonekana kuwa ni ujumbe wa moja kwa moja kwa Harmonize, Kajala amejirekodi akiwa ndani ya gari huku akiimba Wimbo wa Rayvanny na Zuchu wa I Miss You.
Kajala amechagua kuposti akiimba kipande cha wimbo huo kinachosema; “Sipendi tuchukiane, japo najua Mungu amenilinda na Mengi na sisemi sisemi turudiane, hilo tambua miye nilipovunja sijengi na niliko salama…”

Huenda hiyo ni njia ya malkia huyo wa Bongo Movies kumjibu Harmonize baada kujaribu kunyamaza kwa wiki mbili tangu sakata hilo lilipoanza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad