Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imetoa ufafanuzi kuhusiana na Hali ya Matairi ya Ndege zake


Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imetoa ufafanuzi kuhusiana na habari iliyosambaa mitandaoni kuhusu hali ya matairi ya ndege zake ambayo inadaiwa kuwa hali yake inahatarisha usalama wa ndege na abiria.

"ATCL inamshukuru abiria huyu kwa kuonesha umakini kwa usalama wa abiria na ndege, ATCL hufanya ukaguzi wa lazima wa ndege zake zote katika maeneo yote ya ndege yakiwemo matairi baada ya safari zote za siku, kabla ya kuanza safari za siku na baada ya kila safari"

"Kwa mujibu wa rekodi zilizowekwa na ATCL, tairi ya ndege tajwa lilikuwa na mruko mmoja tangu tangu kubainika kulika kwa tabaka la kwanza hivyo kulikuwa na miruko saba zaidi hadi kufikia saba zaidi hadi kufikia ukomo wa matumizi yake kwa mujibu wa miongozo"

"Kwa misingi hiyo tairi hilo lilikuwa bado ni salama kutumia kwa mujibu wa miongozo iliyowekwa na Waundaji na kufuatwa na ATCL"

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad