BARABARA kadhaa zimefungwa karibu na mahakama ya Pietermaritzburg huku kesi ya ufisadi inayomkabili Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma ikiendelea leo Jumatatu.
Zuma anakabiliwa na mashtaka mengi ya ulaghai na utakatishaji fedha yanayohusiana na mkataba wa silaha wa miaka ya 1990 na kampuni ya Ufaransa.
Julai mwaka jana, maandamano ya ghasia yalizuka katika baadhi ya maeneo ya Afrika Kusini baada ya Zuma kukamatwa.
Changamoto nyingi za kisheria zimesababisha ucheleweshaji wa muda mrefu na kuahirishwa kwa kesi hii inasubiriwa kwa hamu sana.
Leo mawakili wa Zuma watajibu hati ya kiapo ya mwendesha mashtaka, ambayo inataka kuwasilisha ushahidi mpya.