Kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 13 yuko mbioni kupata degree yake ya shahada ya kwanza mwaka huu, kutokea Chuo Kikuu cha Minnesota, nchini Marekani.
Kijana huyo aitwaye Elliott Tanner, atapata degree yake baada ya kujikita kwenye masomo ya fizikia na hesabu na kwa sasa ana wastani wa GPA ya 3.78.
Tayari amekubaliwa katika programu ya PhD ya Fizikia ya Chuo Kikuu cha Minnesota na ana mpango wa kuwa mwanafizikia wa nadharia ya juu na kuwa profesa shuleni "Nina shauku ya ajabu ya fizikia,imekuwa moja ya mambo ninayopenda kufanya."
Tanner alianza kusoma na kufanya mazoezi ya somo la hesabu akiwa na umri wa miaka 3, kulingana maelezo ya mama yake Michelle Tanner, alimaliza masomo ya secondary na na shule ya upili katika mda wa miaka 2 tu na kuanza chuo kikuu akiwa na umri wa miaka 9 baada ya kusomea nyumbani kwao.
Hata kwa mafanikio yake ya ajabu, kijana huyu hatokuwa Mhitimu mdogo zaidi wa Chuo Kikuu kikuu, Cheo hicho kinashikiliwa na Michael Kearney, ambaye alipata stadhahada yake ya kwanza katika somo la anthropolojia kutoka Chuo Kikuu cha Alabama Kusini nchini Marekani mwaka 1994, alikuwa na umri wa miaka 10 tu.