Kimenuka..Wanajeshi wa Uingereza Wadakwa na Urusi Wakiipigania Ukraine



WANAJESHI wawili wa Uingereza waliokuwa wakipigana nchini Ukraine wamekamatwa na majeshi ya Urusi, ambapo wameoneshwa kwenye televisheni ya serikali ya Urusi wakimuomba Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson kuwasaidia warudi nyumbani.

Gazeti la Uingereza la The Guardian limeripoti Jumatatu Aprili 18 kuwa, Shaun Pinner na Aiden Aslin wameomba kubadilishwa na mwanasiasa Viktor Medvedchuk, anayeiunga mkono Urusi, ambaye amekuwa kizuizini nchini Ukraine tangu wiki iliyopita.

Wakati huohuofamilia ya mwanajeshi wa zamani wa Jeshi la Uingereza, aliyekamatwa na majeshi ya Urusi katika mji uliozingirwa wa Mariupol, imewataka waliomkamata kumchukulia kama mfungwa wa kivita kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo (FCDO), familia ya Shaun Pinner ilieleza jinsi alivyohusika katika utetezi wa Ukraine, ambayo walisema ni kama "nchi yake nyingine".

Taarifa hiyo ilisomeka hivi: “Shaun alikuwa mwanajeshi aliyeheshimika sana ndani ya Jeshi la Uingereza, akihudumu katika Kikosi cha Royal Anglian Regiment kwa miaka mingi. Alihudumu katika ziara nyingi zikiwemo Ireland Kaskazini na Umoja wa Mataifa nchini Bosnia.”

Pinner, 48, alionyeshwa katika runinga ya Urusi mwishoni mwa juma na kusema alikuwa akipigana pamoja na wanamaji wa Ukraine, wakati vikosi vya Vladimir Putin vilipovamia karibu wiki nane zilizopita.

Mwanajeshi huyo wa zamani katika kikosi cha Kifalme cha Uingereza, ambaye alionekana amechoka kwenye video hiyo, alisema alikuwa akipigana katika mji huo uliozingirwa kwa muda wa wiki tano, lakini sasa yuko katika eneo lililojitenga la Donetsk.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad