Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara, leo Aprii 5, 2022 imeahirisha tena kesi ya mauaji inayowakabili maafisa saba wa polisi hadi itakapotajwa tena Aprili 19, 2022.
Akiahirisha kesi hiyo, Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Mussa Essanju amesema upelelezi wa kesi hiyo namba 1/2022 haujakamilika.
Amesema watuhumiwa walipopewa nafasi ya kujieleza wamedai kutokuwa na hoja yoyote ya kuiambia mahakama.
Kesi hiyo inawakabili maafisa saba wa polisi wakituhumiwa kumuua mfanyabiashara wa madini Musa Hamis Hamis (25) Januari 5, 2022.