Kinachomkuta Harmonize Kurudiana na Kajala si KIPYA katika ulimwengu wa mapenzi

 


Katika kuperuzi mtandaoni nimekutana na habari zinazotrend zinazomuhusu mwanamuziki Harmonize aka Bakhresa kuwa anapigana juu chini ili aweze kurudiana na muigizaji Kajala.

Kwa haraka haraka mtu anaweza kusema kuwa Harmonize anatafuta kiki ili atrend mitandaoni ila kwa jicho la mbali ukitazama unaweza kuona kuwa hiyo sio kiki ila kijana Bakhresa ameleweshwa kimapenzi na huyo (Kajala).

Harmonize amejitahidi kuukimbia ukweli wa kimapenzi kwa kwenda zake kuanzisha penzi jipya na mwanamke kutoka Australia ila bado moyo wake umekataa kusonga mbele, badala yake umebaki katika gereza la Kajala.

Mwanaume kuna kipindi unaweza ukapita kwa wanawake wengi ila ukanasa katika tundu bovu la mwanamke mmoja na hapo ndio utajikuta huchomoki maana moyo umeshanasa.

Kabla ya kusema kuwa ni kiki, tujiulize Harmonize alipewa nini na huyu mwanamama Kajala kiasi moyo wake umeshindwa kusonga mbele??

Harmonize tayari ni star mkubwa Tanzania na Africa kwa ujumla, hivyo haihitaji kiki za Kajala ili mziki wake usonge mbele, ila nachojua hii hali anayopitia Harmonize watu wengi sana wamepitia katika safari ya mapenzi, kumwacha huyu alafu baadae unakuja jutia 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad