Kinda wa Kitanzania Kelvin John (19) ambaye alipandishwa na kuingizwa kwenye Timu ya wakubwa ya KRC Genk ya Ubelgiji jana amecheza mechi yake ya kwanza jana katika ushindi wa 5-0 vs Eupen ikiwa ni mechi ya Ligi Kuu Ubelgiji.
Kelvin John katika mchezo huo aliingia akitokea benchi dakika ya 81 kuchukua nafasi nafasi ya Mjapan Junya Ito na kwenda kumalizia dakika 9 zilizosalia “Nashukuru sana Mashabiki kwa sapoti nikicheza mchezo wangu wa kwanza KRC Genk, nafuraha sana asanteni wote” ——— @kelvin.p.john