Kiongozi wa kundi la Al-Qaeda Ayman al-Zawahri, ameonekana kwenye mkanda wa nadra wa vidio akimsifu mwanamke wa Kiislamu nchini India, ambaye mwezi Februari alipinga marufuku ya kuvaa hijab, na kufichua ushahidi wa kwanza katika miaka kadhaa kwamba bado yupo hai.
Uvumi wa kifo cha al-Zawahri umeenea kwa zaidi ya miaka miwili, lakini katika mkanda huo wa vidio uliotolewa jana Jumanne na kutafsiriwa na kundi la Intelijensia la SITE, kiongozi huyo wa Al-Qaeda anamsifu Muskan Khan, ambaye alikaidi marufuku ya kuvaa hijab katika shule iliyopitishwa na jimbo la kusini mwa India la Karnataka.
Vidio za huko nyuma za Zawahri hazikuweza kubainisha wazi muda ambao zilirekodiwa, na kuchochea uvumi kuhusu kudorora kwa afya yake na hata kifo chake. Zawahri alichukua uongozi wa Al-Qaeda baada ya kuuawa 2011 kwa Osama bin Laden na majeshi ya Marekani.
Zawahri amesadikika kuwa katika mikoa ya Kaskazini mwa Afghanistan ya Kunar na Badakhstan, kwenye mpaka na Pakistan