Kisa Basi Kutengenezwa Kwa Vifaa vya Ujenzi, Taboa Waomba uchunguzi Ajali ya Morogoro Urudiwe



Dar es Salaam. Chama Cha Wamiliki wa Mabasi (Taboa) waomba serikali kurudia uchunguzi wa ajali ya basi iliyotokea Morogoro na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 20 na kwamba vifaa vya kwenye gari hilo vilikuwa vifaa rasmi na sahihi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa mawasiliano wa Taboa, Mustafa Mwalongo alisema vifaa vilivyotajwa kuwa havikukithi vigezo kama ‘ringboard’ ni vifaa vinavyotumika na mabaasi yote ya kisasa hata kama na kwenye ujenzi pia hutumika.

“Vifaa kama ringboard vipo kwenye magari yote ya kisasa, kusema ni vifaa vya ujenzi sio sahihi. Tunaomba serikali irudie uchunguzi na sisi tushrikishwe” alisema na kuongeza kuwa ripoti iliyotolewa na serikali haikuwa sahihi.

Taboa kupitia mwekahazina wake Issa Nkya waliomba serikali kusimamia sheria ifuate mkondo wake na waliofanya makosa kwenye ajali hiyo ndio wachukuliwe hatua.


“Serikali imeagiza mmiliki wa gari lile akamatwe, sasa mmiliki anakosa gani? Uchunguzi inabadi ufanyike na sheria ifate mkondo waliofanya makossa ndio watiwe hatiani.

Taboa wanayasema haya siku mbili baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni kutoa ripoti kuwa ajali hiyo iliyosababisha vifo wa Zaidi ya watu 20 ulitokana na uzembe wa matumizi ya vifaa visivyo rasmi kwenye magari

Masauni alinukuliwa na gazeti hili akisema, “Uchunguzi umebaini kulikuwa na vyuma laini ambapo wakati mungine hutumika kutengeneza vitanda lakini walifnga kwenye gari, vingine hutumika kwenye zege kwenye ujenzi wa nyumba lakini viliwekwa kwenye chesis ya gari na ndivyo vilivyokata viungo vya wenzetu”.


Katika hatua nyingine Taboa kupitia kwa naibu mweka hazina wao, Mbazi Mjema walisema wapo tayari kushirikiana na serikali katika uchunguzi na kampeni iliyotangazwa na IGP juu ya kufanya ukaguzi yakinifu kwa muda wa mwezi mmoja.

“Tungependa wafanya hata Zaidi ya mwezi tutatoa ushirikiano. Nitoe rai kwa madereva wote sio wa mabasi pekee juu ya kjuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuokoa maisha ya raia wasio nanhatia” alisema Mjema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad